WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

MWEE ETI MIMBA YA LINAH YACHOROPOKA

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.

Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.

“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.

Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.

“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.
Credits:GPL

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: